Watu watatu wamefariki dunia mkoani Pwani, wawili kati yao
katika ajali ya basi iliyojeruhi wengine wanane
Basi hilo mali ya kampuni ya Modern Coach lililokuwa
likitokea Nairobi kwenda Dar es Salaam, liliacha njia na kupinduka
Ajali hiyo imetokea jana Ijumaa Agosti 3, 2018 saa 5.45
usiku katika Kijiji cha Kimange kwenye barabara ya Segera – Chalinze
Akizungumza leo Jumamosi Agosti 4, 2018, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Pwani, Blasius Chatanda amewataja waliofariki dunia kuwa ni
Aliakimu Mkiganda (41) mfanyabiashara ambaye ni raia wa Rwanda na
Emmanuel Indimuli (3) raia wa Kenya. Miili yao imehifadhiwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH
Amesema majeruhi katika ajali hiyo ni Penina Wango (33),
Aliasgher Morbiwalia (18), Adrian Flovick (19), Mohamed Idris (18) Mita
Naidhukum (54), Adrin Maula (16), Erick Muthon (30) na Hemik Muthon (49)
wote raia wa Kenya
Amesema majeruhi wote walipelekwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) kwa matibabu
Amesema dereva wa basi hilo amekimbia na juhudi za kumsaka
zinaendelea ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake
Katika tukio jingine, amesema mwendesha pikipiki Idd Bakar
(20), amefariki dunia baada ya kugongana na basi mali ya kampuni ya ABC
lililokuwa linatokea Dar esalaam kwenda Mailimoja, Kibaha
Ajali yaua watatu Pwani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment