Dk Kigwangalla ahamishiwa Dar


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ameondolewa katika hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center na kuhamishiwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi

Dk Kigwangalla amepata ajali leo Jumamosi Agosti 4, 2018 eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini

Katika ajali hiyo ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba amefariki dunia

Akizungumza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema licha ya waziri huyo kuendelea vizuri, anahitaji matibabu zaidi

Amesema ndege itakayomchukua waziri huyo ipo Arusha na kwamba ataambatana na watu kadhaa

Kuhusu mazishi ya Temba, amesema  yatafanyika kesho saa saba mchana nyumbani kwao  Masama wilayani Hai mkoani Kilimanjaro

Dk Kigwangalla aliondolewa katika hospitali hiyo akiwa pamoja na Milanzi, mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki

Awali,  waziri huyo alipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Magugu na kuhamishiwa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kwa helkopta
Dk Kigwangalla ahamishiwa Dar Dk Kigwangalla ahamishiwa Dar Reviewed by KUSAGANEWS on August 04, 2018 Rating: 5

No comments: