Mtoto wa
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa Fred Lowassa ni miongoni mwa wanachama
watano wa Chadema waliochukua fomu za kugombea ubunge jimbo la Monduli
Aliyekuwa
mbunge wa jimbo hilo, Julius Kalanga alijiuzulu na kujivua uanachama wa Chadema
na kuhamia CCM
Katibu wa
Chedema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa akizungumza na Mwananchi leo Agosti 9
alisema Fred amechukua fomu na kurejesha
Golugwa ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, aliwataja wagombea wengine ni
Cecilia Ndosi ambaye ni Mwenyekiti Baraza la Wanawake wa Chadema mkoa Arusha na
Diwani viti maalum
Amesema
wengine ni Yona Laizer, Lobulu Kivuyo na Eric Ngwijo
Amesema
wagombea hao watapigiwa kura za maoni katika kikao kitakachofanyika Jumamosi
kata ya Migungani wilaya ya Monduli
“Kikao hicho
kitaratibiwa na ofisi ya Kanda ya kanda ya kaskazini na baadaye majina
kupelekwa kamati kuu,” amesema
Golugwa
amesema katika jimbo la Korogwe vijijini mgombea mmoja amejitokeza ambaye
ni Amina Saguti
Wengine
waliochukua fomu kwa upande wa Korogwe Vijijini lakini
hawakurejesha hadi ulipofika mwisho wa kurudisha fomu ni Aroan Mashuve na
Dafi Dafi
Golugwa
amesema kikao cha kumjadili mgombea huyo kitafanyika Jumapili Korogwe
"Mtoto wa
Lowassa aonyesha nia ubunge Monduli
Mtoto wa Lowassa achukua fomu kuwani ubunge Monduli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment