Mwanafunzi wa kidato cha nne katika
Shule ya Sekondari ya Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi jijini Mwanza,
Mariamu Tabu (18)amefariki dunia kwa kile kilichodaiwa ni kupigwa na baba yake
mzazi baada ya kutohudhuria shuleni.
Akizungumza na wanahabari jana
Agosti 9, Kamanda wa Polisi jijini humo Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kituo cha Misungwi na
atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.
Kamanda Msangi amesema kuwa mama
mzazi wa Mariam, Kija Mashauri amelieleza Jeshi la Polisi kuwa Agosti 6,
mwanaye alikwenda shule lakini hakurudi nyumbani badala yake alirudi Agosti 7
jioni, ndipo baba yake aliuliza alipokuwa na kuanza kumpiga.
“Baba tayari tumemkamata kwa
ushirikiano na wananchi, mara baada ya kutekeleza tukio la kumpiga mwanae
alitaka kukimbia akazuiwa na wanakijiji, ambapo walimuwahisha mtoto katika
zahanati ya kijiji kwakuwa alikuwa katika hali mbaya alifariki akiwa mapokezi”,
amesema Msangi.
Baba Aua Mtoto kwa Kipigo Jijini Mwanza
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment