Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepinga Jeshi la Polisi
kumfungulia mashtaka ya kuandamana bila kibali mwandishi wa habari wa gazeti la
Tanzania Daima, Sitta Tuma
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Agosti 9, 2018 na Kaimu
Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, imeeleza kustushwa na taarifa za
kukamatwa na kupigwa kwa mwandishi huyo wakati akiwa kazini
Inaeleza kuwa jukwaa hilo halikubaliani ya polisi
kumfungulia mashtaka ya kuandamana bila kibali kwa sababu mwandishi huyo
alikuwa kazini
“Mashtaka hayo yafutwe mara moja, Polisi wanapaswa kutambua
na kuthamini kazi ya uandishi wa habari sawa na wao wanavyofanya kazi ya ulinzi
na usalama kwani uandishi ni kazi sawa na kazi nyingine, ”imeeleza sehemu ya
taarifa hiyo
“Tunawasihi polisi kumwachia huru mara moja. Tuma amekamatwa
katika mazingira halali ya mwandishi kufanya kazi”.
Tuma alikuwa anapiga picha katika mkutano wa Chadema
uliokuwa ukifanyika katika Kata ya Turwa, Wilayani Tarime , mkoani Mara
Taarifa hiyo inafafanua kifungu cha (7)(1)cha sheria ya
huduma ya habari (MSA,2016) kinatambua taaluma ya uandishi habari na kinampa
mwandishi haki na wajibu wa kukusanya, kuchakata na kuchapisha taarifa
mbalimbali bila kizuizi
Polisi yawaachia mbunge Matiko, mwandishi
“Viongozi waandamizi wa polisi mara kadhaa wamewaahidi
waandishi wa habari kuwa wanaheshimu uhuru wa vyombo vya habari, waandishi
wanapokuwa kazini , ila kwa mshangao tumeona Tuma akikamatwa kupigwa kinyama
huko Tarime, ”imesema taarifa hiyo
TEF wapinga polisi kumfungulia mashtaka mwanahabari, wataka aachiwe huru
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment