Mke wa Bobi Winne awatoa machozi wanamuziki waliomtembelea


Wanamuziki ambao nchini Uganda wameshindwa kuzuia machozi yao baada ya kufika nyumbani kwa Mbunge Bobi Winne

Wanamuziki hao wakikiwakilisha Chama cha wanamuziki nchini nchini humo (UMA) kimepeleka msaada kwenye familia ya  Winne anayeshikiliwa katika gereza la Makindye kwa madai ya kushambulia msafara wa Rais Yoweri Museveni

Wanamuziki hao walifika nyumbani eneo la Magere anapoishi  mwanamuziki huyo na kumkuta mke wake Barbra Kyagulanyi na kumkabidhi msaada ikiwamo chakula

Mke wa Bobi Wine aliwaeleza wanamuziki hao kwa masikitiko kwamba mume wake anapata tabu sana kwa kuugulia maumivu yaliyotokana na kupigwa na wanajeshi 

Kyagulanyi alisema kwenye waraka wake  kwamba alifanikiwa kumuona mume wake akiwa katika gereza la jeshi la Makindye akiwa katika hali mbaya

Alisema kwamba  alifika gerezani hapo akiwa na watu wa haki za binadamu,mwanasheria wake na akamuona mume wake huyo akiwa hai licha ya kuwa na hali mbaya hivyo anamuomba Mungu amsaidie apone

''Bobi ameumizwa, anamaumivu makali kila sehemu anatia huruma tumuombeeni hawezi kusimama wala kutembea''alisema
Alisema mume wake anaongea kwa tabu sana,anatoa damu puani anahitaji kupatiwa huduma za kipekee chini ya uangalizi wa daktari wake

Mwanamuziki maarufu  Ronald Mayinja wako pamoja na Familia ya mwanamuziki huyo  na kwamba wanatimiza wajibu wao kama ndugu wengine walioguswa na tatizo ambalo limemkuta mwenzao

Baadhi ya wanamuziki maarufu ambao walifika nyumbani kwa Bobi Wine ni pamoja na  Juliana Kanyomozi, Moureen Nantume, Haruuna Mubiru, Spicy Diana, Litto Boss, Rema Namakula, Evelyne Lagu na  Winnie Nwagi.
Mke wa Bobi Winne awatoa machozi wanamuziki waliomtembelea Mke wa Bobi Winne awatoa machozi wanamuziki waliomtembelea Reviewed by KUSAGANEWS on August 20, 2018 Rating: 5

No comments: