Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka
mitano jela aliyekuwa Mhasibu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Gryson Mnyawami
baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa zaidi ya Sh9 milioni akiwa mtumishi wa
umma
Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega ametoa hukumu hiyo leo
Agosti 16 baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watano wa upande wa mashtaka
ambao walithibitisha wizi huo pasipo kuacha shaka.
Wakili wa Serikali
Janeth Magoho ameieleza mahakama kuwa mshtakiwa huyo ni mkosaji wa kwanza na
hakuna kumbukumbu za makosa mengine
Hata hivyo, Magoho aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa
mshtakiwa huyo kwa kuwa kitendo cha wizi alichofanya akiwa mtumishi
wa umma ni kibaya na kinaitia hasara Serikali
Ameongeza kuwa, suala la wizi katika Chuo cha ustawi
limekuwa likitokea mara kwa mara
“Kitendo hicho ni kudhulumu wanafunzi na kwamba siyo cha
haki kwani ile fedha ni fedha ya walipa kodi hivyo adhabu kali itakuwa fundisho
kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo,”amesema
Mnyawami katika utetezi wake aliiomba mahakama hiyo
kumpunguzia adhabu na alikubali kulipa fedha hizo taratibu lakini taasisi ndiyo
ilimkatalia
Ameongeza kuomba apunguziwe adhabu kwa kuwa dada yake
ni mgonjwa na mama yake ni mjane na wote wanamtegemea yeye.
Baada ya kusikiliza hoja hizo Hakimu Mtega alimuhukumu
mshtakiwa huyo kifungo cha miaka mitano jela
Mhasibu Chuo cha Ustawi wa jamii atupwa jela miaka mitano
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment