Mfanyabiashara
Davis Mosha anashikiliwa na Idara ya Uhamiaji baada ya jana Agosti Mosi, 2018
kukamatwa kwa madai ya kuwazuia askari wa Idara hiyo kutekeleza majukumu
yao
Akizungumza msemaji
wa idara hiyo, Ali Mtanda amesema Mosha aliwashambulia askari hao na
kumnyang’anya mmoja wao simu ya mkononi baada ya kufika katika jengo la Delina
lililopo Sinza Mori, jijini hapa
"Askari
walifika kwenye majengo hayo na kujitambulisha kwa mlinzi na moja kwa moja
walionyeshwa ofisi za meneja,” amesema Mtanda
“Wakati
wakifanya mazungumzo ya kikazi na meneja huyo, ghafla akatokea Mosha na kuanza
kuwafokea, kisha kuwashambulia na kumnyang'anya askari mmoja simu yake.”
Amesema
alichofanya Mosha ni kinyume cha sheria ya uhamiaji namba 54 kifungu cha 45
kipengele 1 F, kinachozungumzia kumzuia ofisa wa uhamiaji kufanya kazi yake ya
ukaguzi
Mtanda amesema
bado wanamshikilia Mosha kwa uchunguzi zaidi na kama kuna hatua nyingine zitafuata
watatoa taarifa
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Murilo amesema tayari wamepokea taarifa
ya tukio hilo, wanafanya uchunguzi kwa hatua za kisheria
"Tunachunguza
ili kujua kilichotokea ni nini, baada ya hapo ndio hatua nyingine zitafuata,”
amesema Murilo
Mfanyabiashara Dar akamatwa na askari wa uhamiaji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment