Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema serikali
itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wachimbaji wadogo nchini kunufaika ili
iweze kukusanya kodi zitakazotumika kwenye shughuli za maendeleo
Ametoa kauli hiyo leo Agosti 2 wakati akizungumza na
wachimbaji wadogo wa madini aina ya Green Garnet eneo la Lemshuku katika Kijiji
cha Komoro wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara
Amesema lengo la kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo ni
kuwapa nguvu ya kukua kutoka wachimbaji wadogo hadi wachimbaji wa kiwango cha
kati hatua itakayoongeza mapato na ajira.
Kairuki amesema serikali inakamilisha mchakato
wa kurejesha ruzuku kwa wachimbaji wadogo uliokua umesitishwa baada ya
kubainika sio wote waliokua wakinufaika walikua wachimbaji wadogo
"Serikali inaamini kupitia ruzuku tutakayoanza kuitoa
kwa wachimbaji wadogo ambao hawana uwezo wa kifedha watanufaika ipasavyo, lengo
sio mbaki wachimbaji wadogo siku zote,” amesema Kairuki.
Amesema mchango wa sekta ya madini nchini ni asilimia 4.7
kiwango ambacho ni kidogo ukilinganisha na wingi rasilimali hiyo na nguvu kazi
ya vijana wanaoweza kuwa kwenye sekta ya madini
Ameongeza kuwa serikali imeshabainisha maeneo 44 kwaajili ya
wachimbaji wadogo nchini na utaratibu wa kuyatoa utafanyika kwa kufuata
taratibu
Mwenyekiti wa chama cha ushirika wa wachimbaji
wadogo Lemshuku(Komisco),Salehe Abdallah amesema ushirika wao una jumla ya
wachimbaji wadogo 250 na wamekua wakitoa michango mbalimbali ya elimu katika
shule ya Msingi ikiwamo ujenzi wa madarasa mawili na nyumba moja ya walimu
Waziri Kairuki aahidi mazingira mazuri kwa wachimbaji wadogo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment