Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Suleiman Bungara maarufu Bwege
amemtuliza Zitto Kabwe, akimtaka kutokuwa na wasiwasi licha ya Jeshi la Polisi
kufungua jalada la uchunguzi dhidi yake
Jana Agosti Mosi, 2018 msemaji wa jeshi hilo, Barnabas
Mwakalukwa alisema wamefungua jalada la uchunguzi dhidi ya mbunge huyo wa
Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), ikielezwa kuwa alitoa maneno ya uchochezi dhidi
ya viongozi wa Serikali
Kauli hiyo ya polisi imekuja baada ya Waziri wa Mambo ya
Ndani, Kangi Lugola kumtaka Zitto kujisalimisha polisi kwa kuwa ametoa kauli za
uchochezi wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo
la Kilwa Kusini, mkoani Lindi
Akizungumza Bwege amesema Zitto hana makosa kwa kuwa
alimualika jimboni kwake kuzungumza na wananchi, si kuandaa mkutano
“Kama makosa ninayo mimi niliyemualika Zitto. Pale hakuna
kesi yoyote ngoja tuone huo uchunguzi wao utasema nini,” amesema Bwege
Bungara ameeleza namna alivyohojiwa na polisi Julai 30,
2018 siku moja baada ya kufanyika kwa mkutano huo katika viwanja vya
Garden ya Mkapa Kilwa Masoko
Amesema polisi walimhoji mambo mawili, “kwanza ni kwanini
alimualika Zitto kuhutubia mkutano wangu wakati si mbunge wa eneo hilo.
Waliniuliza njia niliyotumia kumualika, nikawajibu nilimuandikia barua
“Niliwaeleza kuwa Zitto alikuja kama mbunge mwenzangu na sio
kiongozi wa chama. Walinieleza kuwa sikufuata utaratibu kwa sababu kibali
changu cha mkutano sikueleza ujio wa Zitto.”
Baada ya kauli la Lugola, Zitto alijibu kupitia ukurasa wake
wa mtandao wa kijamii wa Twitter, akibainisha kuwa atakwenda ikiwa atapewa wito
wa kisheria
Ameandika, “waziri hana hayo mamlaka. Kama polisi wananitaka
watoe wito wa kisheria nitakwenda.”
“Nitaendelea na kampeni za ubunge wa Buyungu ambapo
tunamuunga mgombea wa Chadema na madiwani wa ACT-Wazalendo kwenye kata kadhaa.
Nashauri waziri ampate kwanza yule mbwa wa polisi bandari
Mbunge Bwege amtuliza Zitto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment