Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemtumia rambirambi
Rais John Magufuli kufuatia kifo cha dada yake, Monica
Monica alifariki jana asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya
Bugando jijini Mwanza alikokuwa amelazwa kwa matibabu zaidi
Mbowe pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
ameandika katika ukusara wake wa Twitter akisema, “Kwa niaba ya Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni na wana Chadema wote, natoa pole na salaam za rambi rambi kwa
Mh. Rais @MagufuliJPM kwa kufiwa na dada yake Monica Magufuli.”
“Mungu awape faraja na ailaze roho ya marehemu mahali pema
peponi,” ameongeza Mbowe
Mwanachama wa Chadema, aliyewahi kuwa waziri katika utawala
wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Lazaro Nyalandu ameandika katika twitter yake
akisema, “Natoa pole kwa Mh. Rais @MagufuliJP na familia yake kwa kufiwa na
dada yake mpendwa, Monica Magufuli.”
“Hakika, Maisha yana thamani kubwa. Mungu awafariji na ampe
dada yetu pumziko la milele mahali pema peponi, Amina,” ameongeza Nyalandu
Mwanasiasa mkongwe nchini, Profesa Mark Mwandosya naye
ameandika katika Twitter yake akisema, “Familia yangu na mimi mwenyewe tunawapa
pole Mheshimiwa Rais @MagufuliJP na familia yote Chato na kwingineko kifo cha
mpendwa wenu Bi. Monica Joseph Magufuli.”
Profesa Mwandosya ameongeza, “Mwenyezi Mungu awape subira.
Kwake tulitoka na hakika tutarudi Kwake. Raha ya milele umpe Ee Bwana. Apumzike
kwa Amani
Waziri wa zamani wa maliasili na utalii, Balozi Khamis
Kagasheki kupitia Twitter amesema, “Mh Rais Magufuli @MagufuliJP nakupa mkono
wa pole wewe na family yako kwa kuondokewa na dada yako Bi Monica. Apumzike kwa
amani.”
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),
umetoa rambirambi ukisema, “Pole kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli kwa kuondokewa na dada yake mpendwa Bi.
Monica Joseph Magufuli.”
“Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihidimiwe.
Apumzike kwa Amani,” umeongeza
Mbowe amtumia rambirambi Rais Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment