Mama mbaroni kwa kumuua mtoto wake kwa fimbo


Wanawake wawili wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma mbalimbali akiwamo mmoja aliyemuua mtoto wake wa kiume wa miaka 11 kwa kumpiga fimbo kichwani

Katika tukio jingine mwanamke mwingine anashikiliwa na polisi akituhumiwa kumsokomeza mwiko sehemu za siri mtoto wa dada yake mwenye umri wa miaka sita

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema hayo leo Agosti 14 wakati akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya mkoani humo kwa waandishi wa habari

Kamanda Mutafungwa amesema matukio yote yametokea katika wilaya za Gairo na Manispaa ya Morogoro na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara moja.

Mama mbaroni kwa kumuua mtoto wake kwa fimbo Mama mbaroni kwa kumuua mtoto wake kwa fimbo Reviewed by KUSAGANEWS on August 14, 2018 Rating: 5

No comments: