Kamati Kuu maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM
imewateua Julius Kalanga na Mwita Waitara kuwa wagombea ubunge katika majimbo
walikojiuzulu.
Katika kikao kilichofanyika leo Agosti 14, 2018 ofisi ndogo
za chama hicho jijini Dar es Salaam, Kalanga ameteuliwa kugombea ubunge Monduli
ambako alikuwa mbunge kwa tiketi ya Chadema kabla ya kujiuzulu na kuhamia CCM
Waitara amerejeshwa kuwa mgombea jimbo la Ukonga alikokuwa
mbunge kwa tiketi ya Chadema
Kamati kuu ya CCM pia imemteua Timotheo Mzava kuwania ubunge
Korogwe Vijijini, ambako aliyekuwa mbunge Stephen Ngonyani maarufu Majimarefu
alifariki dunia
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imeshatangaza uchaguzi
katika majimbo hayo utafanyika Septemba 16, 2018
Kamati Kuu kupitia kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli
imewashukuru wananchi waliojitokeza kushiriki katika uchaguzi mdogo wa jimbo Ia
Buyungu na kata 77 na kukipa dhamana chama hicho na wagombea wake na
kuwawezesha kushinda kwa asilimia 100
CCM katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na
Uenezi, Humphrey Polepole imesema kushinda katika uchaguzi ni jambo moja,
kuwatumikia wananchi kwa unyenyekevu, uaminifu na kujitoa kushughulika na shida
za watu ni jambo jingine
CCM yawateua Kalanga, Waitara kugombea ubunge
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment