Maafisa 3 wapewa Off Kwa Ubadhirifu wa Fedha za Magufuli Zaidi ya Sh Milioni 600


Maofisa watatu wa halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wamesimamishwa kazi na mkuu wa Mkoa huo Brigadia Jenerali Marco Gaguti

Amechukua uamuzi huo ili maofisa hao wapishe uchunguzi wa upotevu wa zaidi ya Sh600 milioni ambazo hazikuwakilishwa kama mapato ya halimashauri kuanzia  2016 hadi 2018

Hayo yamebainika jana Ijumaa Agosti 17, 2018 katika kikao maalum cha Kamati ya fedha na mipango ya  halmashauri hiyo cha kujadili taarifa ya  kamati iliyoundwa na  aliyekuwa mkuu wa Mkoa huo

Waliosimamishwa kazi ni Alexander Bashaula ambaye ni mweka hazina wa halmashauri hiyo, Salanga Mahendeka (mhasibu) na  Emanuel Maleo ambaye ni ofisa ushirika, wote wakituhumiwa  kupoteza fedha na kukiuka  viapo vya uaminifu

Katika kikao hicho mkuu huyo wa Mkoa amesema zaidi ya Sh690 milioni  hazikuwasilishwa kama mapato ya halmashauri kuanzia Agosti 2016 hadi Mei 2018, Sh 427 milioni hazikuwasilishwa benki na wakusanya mapato

“Baada ya uchunguzi  wa  kamati ya katibu tawala wa mkoa wa Kagera hivi karibuni ilibainika  kuwa mwenendo wa ukusanyaji wa mapato haulidhishi  na tunachukua hatua kwa wanaopoteza fedha za umma” alisema

Ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuanza kuchunguza  ubadhilifu huo wa mali ya umma  pamoja na kufuatilia  wote kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria

Maafisa 3 wapewa Off Kwa Ubadhirifu wa Fedha za Magufuli Zaidi ya Sh Milioni 600 Maafisa 3 wapewa  Off Kwa Ubadhirifu wa Fedha za Magufuli Zaidi ya Sh Milioni 600 Reviewed by KUSAGANEWS on August 18, 2018 Rating: 5

No comments: