Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuagiza Mkurugenzi
wa Makosa Jinai nchini (DCI) kumkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu kabla ya saa 12 jioni leo
Lugola pia ameagiza kukamatwa kwa wamiliki wa kampuni tatu
zinazodaiwa kuhusika katika mradi wa vitambulisho vya taifa, Gotham's
International Limited, Gwiholoto Impex Ltd na Aste Insurance wanaodaiwa kufanya
udanganyifu na kushindwa kurejesha fedha walizotumia kinyume na utaratibu
Akizungumza na wanahabari leo Agosti 21, Lugola ameagiza
kukamatwa watumishi wote wa Nida ambao wanatuhumiwa katika ubadhirifu wa fedha
za umma wakishirikina na kampuni hizo
“Hizi kampuni zimefanya udanganyifu zikishirikiana na baadhi
ya wafanyakazi,”amesema
Hata hivyo amesema baadhi ya kampuni zilizohusika na
ubadhirifu huo zimeanza kurejesha fedha za umma kwa asilimia 84
Lugola amuagiza DCI amkamate aliyekuwa mkurugenzi Nida
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment