Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) imetoa mwaliko kwa watazamani wa ndani katika uchaguzi mdogo
wa ubunge na madiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018
NEC imealika
waangalizi hao kushuhudia uchaguzi katika majimbo matatu ya Ukonga-Dar es
salaam, Monduli-Arusha na Korogwe Vijijini-Tanga pamoja na kata 23 zilizo
kwenye halmashauri 15 za Tanzania bara
Taarifa ya NEC
iliyotolewa leo Agosti 21,2018 na kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Salvius Nkwera inataka waangalizi hao kuwasilisha maombi kuanzia Septemba 1-9,
2018
Kware amesema
kwa mujibu wa kifungu cha 46 (2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343
na kifungu cha 48 (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani),
Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuendesha uchaguzi mdogo wa
ubunge na madiwani
“Kwa ajili ya
kuweka uwazi katika uchaguzi huo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia
Kanuni ya 18 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015, na Kanuni
ya 14 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za
mwaka 2015,”
“Inapenda
kualika asasi za kiraia na taasisi mbalimbali za ndani zinazotaka kuwa
watazamaji wa uchaguzi katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Septemba 16
2018,” amesema Nkware na kuyataja majimbo hayo kuwa ni Monduli, Korogwe
Vijijini na Ukonga
Amesema asasi
au taasisi zinapaswa kuzingatia masharti yafuatayo wakati wa kuwasilisha
maombi; kuwa na anuani kamili ya asasi husika, anuani ya makazi ya ofisi ya
taasisi husika ilipo, na mahali/sehemu ambapo taasisi husika inafanyia kazi
Pia, shughuli
ambazo zinafanywa na taasisi husika kwa mujibu wa hati ya usajili, kutaja
sehemu ambazo asasi/taasisi inataka kufanya kazi hiyo ya utazamaji, kutaja
idadi ya watu ambao asasi/taasisi itawatumia katika kazi hiyo pamoja na taarifa
zao
Masharti
mengine ni; kutaja majina na namba za simu za viongozi wa taasisi husika kama
yalivyoandikwa katika hati za usajili wa taasisi, ikiwa taasisi inahusisha
watendaji wa kimataifa, wawili lazima wawe Watanzania, kuambatisha nakala/kivuli
cha hati ya usajili wa taasisi husika na mwisho kuambatisha nakala/kivuli cha
katiba ya taasisi/asasi husika
“Taasisi
zitakazopewa vibali vya kuwa watazamaji, zitapaswa kuzingatia mwongozo kwa
watazamaji wa ndani na wa kimataifa ulioandaliwa na Tume kwa mujibu wa Kanuni
ya 24 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015, na Kanuni ya 20
ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani za mwaka 2015,” amesema Nkware.
NEC yaalika waangalizi uchaguzi mdogo wa ubunge, madiwani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment