Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla leo
Jumamosi Agosti 4, 2018 amepata ajali eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata
majeraha sehemu mbalimbali mwilini.
Katika ajali hiyo ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba
amefariki dunia
Akizungumza mwenyekiti wa jumuiya ya hifadhi ya jamii
ya Wanyamapori ya Buruge (WMA), Ramadhan Ismail amesema waziri huyo anapatiwa
matibabu katika kituo cha afya Magugu
Amesema baada ya kupatiwa matibabu katika kituo hicho cha
afya, helkopta imefika eneo hilo tayari kwa kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya
KCMC kwa matibabu zaidi
Amebainisha kuwa Dk Kigwangalla ana maumivu katika mbavu,
kiunoni na hawezi kutembea
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augostino Senga amesema
katika gari hilo alikuwepo Dk Kigwangalla, dereva wake, mwandishi wa habari,
msaidizi wake na mlinzi
Amesema hali ya waziri huyo inaendelea vizuri licha ya kuwa
ameumia mkono wa kulia, kifua na shingo
Amebainisha kuwa Dk Kigwangalla, dereva na msaidizi wake
wanaendelea kupata matibabu kituo cha afya Magugu huku taratibu zingine za
kuwapeleka hospitali kubwa zikiendelea
Mbunge wa viti maalumu (CCM), Ester Mahawe amefika
katika kituo hicho kumjulia hali Dk Kigwangalla na kubainisha kuwa amepata
matibabu katika mkono wake wenye majeraha, anaendelea vizuri
Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, mbunge
wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amempa pole Dk Kigwangalla na
kubainisha kuwa amekwenda kumjulia hali wakati akipita eneo alipopata ajali,
akielekea Babati
“Anaweza kuongea ni uhakika kuwa Mungu atamponya haraka,
sala dua na maombi yenu ni muhimu kwa wote waliokutwa na ajali hii mbaya,”
ameandika Lema
Kigwangalla apata ajali, kuhamishiwa hospitali kwa helkopta
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment