Uongozi wa Kampuni ya Bakhressa (BFPL) umesema unasubiri kwa
hamu mwongozo utakaotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) kuhusu ving'amuzi vilivyoondoa chaneli za ndani baada ya
kukiuka masharti ya leseni
Agosti 13 mwaka huu, Waziri wa Habari,
Sanaa,Michezo,Burudani na Wasanii,Dk Mwakyembe aliitaka TCRA kutoa mwongozo
utakaosadia kampuni za visimbuzi za Azam, Zuku na DSTV zitakavyoweza
kurusha maudhui ya ndani
Hivi karibuni kampuni hizo zililazimika kuacha kurusha
chaneli za ndani baada ya kukiuka masharti ya leseni zao ambayo yanawataka
kurusha maudhui hayo kwa kuyalipia
Meneja Uhusiano wa Bakhressa, Hussein Sufian ameiambia
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, leo Alhamisi
Agosti 16, 2018 kuwa wanausubiri mwongozo huo
Kamati hiyo ya Bunge imeelezwa hayo wakati ilipotembelea
kiwanda cha kusindika matunda na kutengeneza juisi kilichopo Mlandenge wilayani
Mkuranga
Sufian ameeleza hayo wakati akitoa changamoto zinazoikabili
kampuni hiyo na kusema hatua ya Serikali ya kuzitaka Azam kuondoa maudhui ya
chaneli za ndani ni kuwaumiza wananchi
"Tunausubiri kwa hamu mwongozo huu ili wananchi wetu
waondokane na hali ya kumiliki visimbuzi viwili jambo ambalo ni mzigo kwao
“Tunaamini busara itatumika zaidi kurejesha huduma kwa
Watanzania na muafaka utapatikana wa suala hili na tuna imani na
Serikali," amesema Sufiani
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Mhandisi
Stella Manyanya amesema wizara hiyo imelisikia jambo hilo na wanalifuatilia kwa
ukaribu kwa sababu linahusu biashara
"Tutalifuatilia ili kujiridhisha na hatimaye tupate
muafaka. Sasa hivi popote panapohusu biashara lazima tufuatilie na hili la
visimbuzi ni biashara pia," amesema Manyanya
Kampuni ya Bakhressa Yasubiri Muongozo ya TCRA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment