Mkazi wa kijiji cha Kinku tarafa ya Mungaa
wilaya Ikungi , Singida, Editha Kanisi (49) ameuawa kwa kukatwa kwa
kisu cha kukatia majani, (mundu) shingoni na kichwani na mume wake Joseph
Wilbroad (53).
Baada ya Joseph kufanya mauaji hayo wananchi wenye hasira kali
nao walimshambulia kwa silaha na kumuua
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo
Agosti 16 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Sweetbert
Njewike amesema tukio hilo limefanyika jana Agosti 15 mwaka huu usiku saa
mbili huko katika kijiji cha Kinku
Amesema kuwa tukio hilo lilitokea jana usiku wakati
wanandoa hao wakijiandaa kulala na uliibuka mzozo mkali baina yao huku kila
mmoja akimtuhumu mwenzake kuwa si mwaminifu kwenye ndoa
“Kila mmoja alimtuhumu mwenzake kutokuwa mwaminifu katika
ndoa yao,”amesema
Akifafanua zaidi amesema malumbano hayo yalisababisha
mwanaume kuchukua kisu cha kukatia majani kiitwacho mundu na kumkata mke wake
shingoni na kichwani
Amesema Editha alijaribu kukimbia lakini alipotoka nje ya
nyumba yao alianguka chini na kufariki dunia papo hapo
“Watoto wao baada ya kuona mama yao kaanguka chini, walianza
kupiga kelele za kuomba msaada na majirani walifika mara moja kwenye eneo la
tukio na wakamwomba Joseph afungue mlango,” amesema Kamanda huyo
"Joseph alikaidi kufungua mlango na ndipo walipouvunja
kwa nguvu.Walipofanikiwa kumkamata Joseph,walimpiga kwa silahaza jadi na
kusababisha kifo chake,”ameongeza.</p></div><div><p>Amesema
uchunguzi zaidi na msako mkali unaendelea kuwasaka waliohusika na mauaji ya
Joseph
Amuua mke wake kwa mundu, Naye Auwawa na Wananchi Wenye Hasira Kali
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment