IGP SIRRO ATOA ONYO KALI KWA MAJAMBAZI WANAOTUMIA SILAHA.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ametoa onyo kali kwa majambazi na wahalifu wengine hususani wanaotumia silaha za moto kuacha mara moja kabla ya kukutana na moto mkali wa Jeshi la Polisi ambapo ametoa wito kwa wazazi kuwakanya watoto wao kujihusisha na vitendo hivyo.
 
IGP Sirro ameyasema hayo Mto wa Mbu Tarafa ya Manyara Wilayani Monduli wakati akizungumza na wananchi wa maeneo hayo ambayo hivi karibuni kulijitokeza mauaji ya wanawake ambapo hivi sasa hali ni shwari..

 Aidha amewataka Viongozi wa Vijiji na Kata kuhakikisha kuwa suala zima la ulinzi na usalama linatiliwa mkazo ili kuhakikisha hakuna mhalifu katika maeneo yao

Kwa upande wao wananchi mbalilmbali wa Mto wa mbu wametoa maoni yao huku wakiahidi kuchangia ujenzi wa kituo cha Polisi ili kuboresha usalama katika eneo hilo ambalo ni muhimu kwa utalii nchini.

Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Mto wa Mbu Bi. Kuluthum Hassan alisema Wahalifu wanaouza bangi, pombe ya gongo na dawa za kulevya wanaendelea kuwafuatilia ili wafikishwe katika vyombo vya dola.

IGP anaendelea na ziara yake katika Wilaya ya Karatu ambapo amezungumza na Askari Polisi katika kuboresha utendaji wa Jeshi hilo.
IGP SIRRO ATOA ONYO KALI KWA MAJAMBAZI WANAOTUMIA SILAHA. IGP SIRRO ATOA ONYO KALI KWA MAJAMBAZI WANAOTUMIA SILAHA. Reviewed by KUSAGANEWS on August 16, 2018 Rating: 5

No comments: