Dc Hai agawa Kifurushi cha Masaa 48 Kwa Boss na Mwanasheria wa Kampuni ya Tudeley Estates Ltd


Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameamuru kukamatwa kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Tudeley Estates Ltd, Jensen Natal na Mwanasheria wa kampuni hiyo, Edward Mroso kwa tuhuma za kukwepa kodi ya serikali kiasi cha zaidi ya Sh800 milioni

Pia ameiamuru Idara ya Uhamiaji Wilayani humo kumnyang'anya hati ya kusafiria meneja wa kampuni hiyo, Trevor Gifford hadi fedha hizo zitakapolipwa.

 Kampuni ya Tudeley inamiliki na kuendesha mashamba ya ushirika ya chama cha msingi cha Murososangi yenye ukubwa wa ekari 2,054.

 Ole Sabaya, ametoa maagizo hayo leo Agosti 16 wakati alipofanya ziara ya kutembelea mashamba ya kampuni hiyo huku akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Hai

Pia aliambatana na Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wilayani Hai, Spécioza Owere

Kabla ya kuingia katika lango kuu la kampuni hiyo Ole Sabaya aliamuru Gifford aitwe huku akiwa na hati yake ya kusafiria na  baadaye akaingia katika ofisi za kampuni hiyo

Akizungumza katika eneo la tukio, Ole Sabaya amesema kwamba ana taarifa za  uhakika kwamba kampuni hiyo imekuwa ikikwepa kulipa kodi ya serikali kwa muda wa miaka saba hadi sasa

Ole Sabaya amesema kwamba kampuni hiyo imekwepa kulipa kodi ya serikali zaidi ya Sh800 milioni ambazo ni malimbikizo ya kodi ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA

Akitoa maagizo hayo Ole Sabaya aliliamuru jeshi la polisi Wilayani humo kumkamata Natal  na Mroso na kuwekwa mahabusu  kwa saa 48 na wahakikishe fedha hizo ambazo ni kodi ya serikali zinalipwa

"Wewe utaenda ndani ili uje uniambie kuna utaratibu gani wa kodi ya serikali kulipwa na ijumaa asubuhi uwepo ofisini kwangu uniambie kodi ya serikali italipwaje,” amesema kuongeza

"Chukua passport yake ya zamani na sasa nataka pésa hiyo ilipwe ndani ya siku saba na TRA niletewe maelezo hayo.”

Mara baada ya agizo hilo maofisa wa jeshi jeshi la Polisi Wilayani humo walimkamata Natal na Mroso na kisha kuwapéleka kwenye gari huku maofisa wa idara ya Uhamiaji wakichukua hati ya kusafiria ya Trevor

Kabla ya Mroso kushikiliwa alimweleza Ole Sabaya kwamba uongozi wa kampuni hiyo ulishawasilisha maombi mbele ya ofisi yake kuwaomba TRA wakague hesabu na madeni ili waweze kulipa

Dc Hai agawa Kifurushi cha Masaa 48 Kwa Boss na Mwanasheria wa Kampuni ya Tudeley Estates Ltd Dc Hai agawa Kifurushi cha Masaa 48 Kwa Boss na Mwanasheria wa Kampuni ya Tudeley Estates Ltd Reviewed by KUSAGANEWS on August 16, 2018 Rating: 5

No comments: