Chama cha Mapinduzi Wilaya ya karatu
kimeonya baadhi ya watendaji wanaohujumu miradi ya maendeleo ikiwemo
miradi ya maji ,barabara ambayo inalenga kutatua changamoto za wananchi.
Mwenyekiti wa Ccm Wilayani hapo
Lucian Akonaay amesema Kuwa wanaohujumu miradi watachukuliwa hatua kwani
wananchi bado wana imani na chama hicho katika kuhakikisha kuwa wananchi
wanapata huduma muhimu za kijamii ikiwemo maji na miundombinu ya barabara
pamoja na huduma za afya.
Akonaay Amesema kuwa chama hicho
kimeandaa utaratibu wa kutembelea miradi ya maendeleo na kujihakikishia
kuwa iwapo inatekelezwa kwa viwango stahiki na kwa wakati uliopangwa
Katibu wa CCM Karatu Solomon
Itunda amesema Kuwa viongozi wa chama wamekua wakikagua maendeleo ya miradi
pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora ikiwa ni pamoja na
kutoa mapendekezo kwa viongozi wa serikali.
Diwani Mteule wa kata ya Baray
kupitia Chama hicho Elitumaini Rweyemamu amesema kuwa wamejiandaa
kusimamia utekelezaji na kutatu kero za wananchi ili kuboresha huduma za
kijamii.
Kwa Upande wake Mkazi wa Karatu
ameipongeza serikali kwa kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa kuchimba visima na
kuiomba iongeze visima na mabomba hususan kwenye maeneo yenye watu wengi
CCM KARATU YAONYA WANAOHUJUMU MIRADI YA MAENDELEO.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment