IGP afanya mabadiliko Jeshi la Polisi


Mkuu wa Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo kwenye jeshi hilo na  kumuondoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (DCP) Ahmed Msangi na  kumhamishia makao makuu ya jeshi hilo

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano Agosti 15, 2018 na Msemaji wa polisi, Barnabas Mwakalukwa imeeleza kuwa Msangi amehamishiwa makao na kuwa Mkuu wa kitengo cha makosa dhidi ya binadamu makao ya upelelezi Dar es Salaam

Mwakalukwa amesema nafasi ya Msangi imechukuliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shana

“Nafasi wa Shana imechukuliwa na Kamanda Wankyo Nyigesa aliyekuwa mkuu wa operesheni kanda maalumu ya Dar es Salaam,” amesema Mwakalukwa

Kwa mujibu wa Mwakalukwa mabadiliko ya uhamisho huo ni ya kawaida yanatokea ndani jeshi la polisi katika kuongeza ufanisi kwenye utendaji kazi

IGP afanya mabadiliko Jeshi la Polisi IGP afanya mabadiliko Jeshi la Polisi Reviewed by KUSAGANEWS on August 15, 2018 Rating: 5

No comments: