Mkataba huo Leo tar 14 August 2018 umesainiwa na
Mkurugenzi wa maji na Usafi wa mazingira AUWSA Bi Ruth Koya pamoja na Kampuni
ya Beijin Constuctioni Mbele ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame
Mbarawa ambapo ni kuhakikisha wanawaondolea wananchi adha hiyo inayowakabili.
Akizungumza Mkurugenzi wa AUWSA Bi Ruth Koya amesema mradi
huo utagharimu fedha za Kitanzania Bilioni 476 na kati ya fedha hizo Sh Bilioni
429 ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo afrika AfDB ambapo
Bilioni 47 ni mchango wa Serikali.
Amesema Lengo la mkataba huo ni kuongeza huduma ya
uondoaji wa majitaka kutoka asilimia 7.66 ya jiji la Arusha hadi kufikia
asilimia 30 na wananchi 4500 wataunganishwa kwenye mfumo wa uondoaji wa
majitaka ambapo jumla ya Bomba zenye km 176.5 zitatumika.
Kwa upande wa Waziri wa maji na Umwagiliaji Prof Makame
Mbarawa amesema mradi huo unatakiwa kutekelezwa ndani ya miaka miwili kuanzia
14 Agost 2018 na kukamilika 13 Agost 2020 na muda wa miezi 12 kwa ajili ya
matazamio.
Hata hivyo ametoa rai kwa mkandarasi wa kampuni hiyo ya
Beijin Construction kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kwa wakati na inatakiwa
ifanyike usiku na mchana kwa kuwa tayari fedha zipo kwa ajili ya mradi huo
Amesisitiza kuwa serikali kufanya hivyo ni kwa ajili ya
kuboresha hali ya upatikanaji wa majisafi na kuboresha Huduma ya uondoaji wa
maji taka katika jiji la Arusha ili kuboresha afya ya hali ya maisha yaw a kazi
wa jiji la Arusha na kwa ujumla wake.
Bilioni 476 kuwaondolea Wananchi Kero ya Maji Jiji la Arusha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment