Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na mbunge wa Tarime
Vijijini, John Heche amesema hata wapinzani wote wakikimbilia CCM, mapambano ya
wananchi kupigania haki zao hayataisha
Pia amehoji kama aliyekuwa mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara
aliyehamia CCM ameondoka kwa sababu ya uenyekiti wa Freeman Mbowe, ataweza
kumtoa Rais John Magufuli kwenye uenyekiti wa CCM?
“Ngoja nimuulize Waitara, kama ameondoka Chadema kwa sababu
ya mwenyekiti na ameshindwa kumtoa Mbowe, ataweza kumtoa Magufuli?” amehoji
mbunge huyo
Heche aliyasema hayo jana akizungumzia kujiuzulu na kuhamia
CCM kwa Waitara
Julai 28, Waitara alitangaza kujivua ubunge na kuhamia CCM
akitaja sababu mbalimbali ikiwamo uenyekiti wa Mbowe
Pamoja na Waitara, mbunge wa Monduli (Chadema), Julius
Kalanga naye alitangaza kujiuzulu uanachama na wadhifa wake
Akizungumza katika mkutano maalumu wa Jimbo la Ukonga, Heche
alisema nia ya Chadema siyo kuwapa watu ubunge isipokuwa kuhakikisha
inawasimamia wananchi katika kupata huduma bora ikiwamo elimu, afya,
miundombinu na uchumi imara
Alisema wananchi wa Ukonga walikesha siku tatu kupigania
ushindi wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, lakini matokeo yake,
Waitara amekimbia mapambano. “Hata kama CCM itanunua wapinzani wote, bado
Watanzania wataendelea na mapambano, yeye ameenda kwa sababu ya masilahi yake
lakini huku nyuma ameacha jeshi kubwa na tutampata mpambanaji mwengine
atachukua jimbo,” alisema Heche
“Niwaambie tu CCM hata mkininunua Heche leo, wananchi
wataendelea kudai maendeleo yao, mtakuwa mmeninunua mimi hamjainunua Chadema.”
Kuhusu hoja ya Waitara kuwa Mbowe amekaa madarakani kwa muda
mrefu, mbunge huyo alisema ni matakwa ya wanachama na sio ya CCM
Alieleza kuwa katiba ya Chadema haijaweka ukomo wa uongozi
na ataendelea kushikilia nafasi hiyo mpaka wanachama watakapotaka kumuondoa.
“Kwani Mwalimu Nyerere (Julius) aliongoza kwa muda gani? Kwani Mbowe aliyeanza
kuongoza mwaka 2006 amefikisha muda wa Mwalimu? Si bado? Basi nyie wanachama
ndio wenye mamlaka na ndio mtakaomuweka mwenyekiti wa masilahi ya chama,”
alisisitiza
Heche alisema ni ajabu kuona kuwa Waitara anaondoka akidai
moja ya sababu ni Mbowe kuongoza chama muda mrefu
Alidai kuwa Waitara ni mwanasiasa wa siasa za mpasuko
“Nimesikia anataka kuja Tarime kupambana na mimi mwaka 2020,
namsubiri kwa hamu, siwezi kupambana na mamluki na haniwezi,” alisema
“Ninawaambia wale wanaotaka kuondoka, milango ipo wazi,
Chadema itaendelea kuwa imara.”
Diwani alia kupakaziwa
Awali, diwani wa Pugu, Boniventure Mphuru alidai
kusikitishwa na taarifa zinazoenezwa kwamba naye ni miongoni mwa viongozi wa
Chadema wanaotaka kuhamia CCM
“Wananchi wa Ukonga puuzieni taarifa hizo, hazina ukweli kwa
sababu sijawahi kuwa CCM, sitaenda na sijafikiria kwenda huko,” alisema
Kwa upande wake, mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Ukonga,
Omary Swea alisema vitisho vya wabunge na madiwani kuhama chama hicho
haviwatishi kwa sababu bado wako imara
Alisema mkutano wa wanachama wa jimbo hilo walioufanya ni wa
kawaida na upo kwenye katiba ya chama chao
Naye mwenyekiti wa Mkoa wa Ilala wa chama hicho, Makongoro
Mahanga alisema pamoja na vita waliyo nayo hawatakata tamaa wala kurudi nyuma
Mdee ahojiwa polisi
Wakati huohuo, mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, baadhi
ya wanachama na wafanyabiashara wa eneo hilo walikamatwa na kuhojiwa na polisi
jana, kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali.
Mdee ambaye pia ni
mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), alisema alipigiwa simu na
vijana wanaofanya biashara ya kutengeneza bustani eneo la Mzimuni lililopo Kawe
kwamba wamepewa notisi ya kuondoka
Alisema wakati anapigiwa simu alikuwa Kunduchi katika ziara,
hivyo ikamlazimu kwenda kuwasikiliza wananchi wake
“Nilipofika nilizungumza nao na kuwaeleza suala hili
nalishughulikia, kwani nimewasiliana na Wizara ya Ardhi; (Idara ya) Mipango
Miji na Tarura (Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini),” alisema.</
“Ni kweli wale vijana wako eneo la barabara na wamenieleza
hawana tatizo la kuondoka, lakini wanahitaji kuelekezwa wapi watakwenda
kuendelea na shughuli zao.”
Mdee alisema baada ya kumaliza kuzungumza na vijana hao,
aliondoka lakini alipofika mbele akaelezwa kuna watu wamekamatwa eneo alilotoka
“Nikaona nirudi, nilipofika nikakuta wanarushwa kichura
chura, nikahoji kuna nini sikupata majibu yanayoeleweka.”
Mdee alisema baada ya hapo, ikaelezwa kuwa vijana hao
waliokuwa chini ya ulinzi watapelekwa kituo cha polisi Kawe na yeye akasema
anatangulia kituoni
“Nilipokuwa nakwenda kama mita 20 nikaambiwa na wewe
mheshimiwa rudi, niliporudi nikaambiwa niko chini ya ulinzi na kuniweka katika
gari yao, tukaenda hadi kituoni na kuhojiwa kwa kufanya mkusanyiko usiokuwa na
kibali,” alisema mbunge huyo
“Baada ya kuhojiwa, mimi na wale vijana lakini na wanachama
wa Chadema wote tumeachiwa na tutajulishwa tena kama tutahitajika.”
Alipoulizwa juu ya kukamatwa kwa watu hao, kamanda wa Polisi
Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jumanne Murilo alikanusha akisema kazi ya Jeshi la
Polisi ni kutoa huduma za kiusalama kwa mtu yeyote, hivyo si ajabu kwa kiongozi
wa chama kufika katika kituo cha polisi inapobidi
“Mtu yeyote akifika kituoni ina maana amekamatwa? Huyo
Makene au Mbowe au Mdee akifika kituoni maana yake amekamatwa? Hilo ndilo swali
langu,” alihoji
“Hivyo watu wasitumie Jeshi la Polisi kujipatia umaarufu
Heche amjibu Waitara uenyekiti wa Mbowe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment