Halima Mdee awaponza wananchi wake

Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Halima Mdee (Mb) pamoja na viongozi wengine, wanachama na wapenzi wa CHADEMA Jimbo la Kawe takribani 13, wamekamatwa na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Polisi Kawe. 

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Tumaini Makene imesema kwamba hadi sasa jeshi hilo halijatoa taarifa rasmi kueleza sababu ya kumshikilia mbunge huyo pamoja na wananchi wake baada ya kuwakamata maeneo ya Tanganyika Parkers, Kawe, jijini Dar es Salaam.

Akielezea kuhusu Mdee kukamatwa Makene amesema kwamba, "awali, Mdee ambaye ni mbunge wa Jimbo la Kawe, alisimamishwa na wananchi alipopita maeneo hayo, wakitaka kumpatia kero zao. Baada ya kusikiliza malalamiko ya wapiga kura wake na kuondoka, inadaiwa polisi walifika eneo hilo na kuanza kuwakamata walioonekana kuwa na sare za CHADEMA".

Ameongeza kwamba alipopata taarifa hizo, Mdee alilazimika kurudi ambapo polisi hao wakiongozwa na askari polisi mwenye cheo cha Inspekta walimuamuru Mdee na viongozi hao kuelekea kituoni. Hadi sasa viongozi hao bado wako kituoni hapo".

Hata hivyo juhudi zinafanyika za kuweza kuzungumza na jeshi la Polisi Kawe ili kujua sababu za viongozi na wananchi hao kukamatwa
Halima Mdee awaponza wananchi wake Halima Mdee awaponza wananchi wake Reviewed by KUSAGANEWS on August 01, 2018 Rating: 5

No comments: