Mkazi wa Pasiansi, Mwanza Prosper Lema, anashikiliwa na
polisi kwa mahojiano akidaiwa kujiteka na kutoa taarifa kwa ndugu akiwataka
watoe Sh5 milioni kama malipo ya kuachiwa huru
Taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi
kwa vyombo vya habari imesema tukio hilo lilitokea Julai 18
“Mtuhumiwa alituma ujumbe mfupi wa maneno kwa njia ya simu
kwa ndugu zake akiomba atumiwe Sh5 milioni ili aachiwe na watu aliodai
walimteka alipokuwa akitembea kwa miguu katika barabara ya Kenyata katikati ya
jiji la Mwanza,” amesema Kamanda Msangi
Amesema baada ya kupokea ujumbe huo, ndugu walitoa taarifa
Kituo cha Polisi Kirumba ndipo makachero wa polisi walipoanza kufuatilia
mawasiliano ya simu iliyotumika kutuma ujumbe huo na kubaini mtumaji alikuwa
eneo la Ngudu wilayani Kwimba wakati akituma ujumbe
“Makachero hao walifanikiwa kumpata mtuhumiwa akiwa
amejifungia peke yake moja ya vyumba vya nyumba za kulala wageni akiwa na
simu ya kiganjani iliyotumika kutuma ujumbe akiomba atumiwe fedha,”
amesema
Kamanda huyo amesema kitendo cha mtuhumiwa licha ya kuzua
taharuki na hofu miongoni mwa ndugu, pia ni kinyume cha sheria
“Kwa hivyo mtuhumiwa atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria
kwa hatua zaidi mara upelelezi wa awali utakapokamilika,” amesema
Atiwa mbaroni kwa ‘kujiteka’ na kuomba Sh 5milioni kwa ndugu zake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment