Na Is-haka, Zanzibar.
Kauli hiyo aliitoa mara baada ya
kuwasili kisiwani Pemba katika mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha
ambapo amezungumza na wanachama mbalimbali katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari
ya Fidel Castro Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema kutokana na uimara huo
hakuna chama kingine mbadala wa Chama Cha Mapinduzi kinachoweza kushuka kwa
wananchi nyumba kwa nyumba na kuratibu kero zao kisha kuzitafutia ufumbuzi wa
kudumu.
Dk.Bashiru aliwahakikishia wanachama
na viuongozi hao kuwa CCM bado ipo imara na itapata ushindi wa kihistoria mwaka
2020 kwa nchini nzima kuliko ushindi unaopatikana kwa sasa katika uchaguzi
mdogo unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.
Aliongeza kwamba sababu za kushinda
na kusambaratisha upinzani zipo kwani vyama vya upinzani nchini vimekosa
muelekeo na ndio maana wanachama wake wanahamia CCM kwa wingi.
Alisema Tanzania inahitaji vyama vya
siasa imara vitakavyolinda na kuhubiri misingi ya utaifa na umoja na msikamano
wa Tanzania, bila ya kujali tofauti za kisiasa.
Kupitia mkutano huo aliwambia
wanachama wa vyama vya upinzania kisiwani Pemba kwamba huu ndio wakati wao wa
kujitawala kifikra kwa kujiunga na CCM kwani Chama Cha CUF hakina tena mvuto
kwa jamii kutokana na tabia ya unafiki na uongo inayofanywa na viongozi wakuu
wa Chama cha CUF.
“Wanachama wa vyama vya upinzani
njoo CCM huku tupo shwari na tumekamilika kila idara wala msihofu chochote
hakuna mtu yeyote wa kuwagusa, na wale wote waliojiunga na chama chetu leo
nahakikishieni kuwa mtafaidika na siasa safi na demokrasia iliyotukuka.
Pia Wana-CCM wenzangu awa wenzetu
wanaojiunga na CCM wapokeeni na kuwathamini kwani wamefanya maamuzi sahihi
ambayo hawatoweza kuyajutia.”, alisema Dk.Bashiru.
Dk.Bashiru kupitia mkutano huo
alitangaza rasmi kuwa Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuvunja ngome zote za
upinzani kabla ya mwaka 2020, kutokana na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya mwaka 2015/2020.
Alisema dhamira ya tasisi hiyo kwa
sasa ni kuendeleza kwa vitendo mambo mema yaliyoasisiwa na vyama vya ukombozi
vya ASP na TANU vilivyoungana na kuzaliwa kwa CCM.
Pamoja na hayo aliweka wazi kuwa
kila kila mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi anatakiwa kulinda Muungano,
Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwani tunu hizo ndio chimbuko la mafanikio
yaliyopo hivi sasa.
Kupitia mkutano huo pia Dk.Bashiru
aliwapokea wanachama wapya 62 waliotoka chama cha CUF na kujiunga na CCM
kisiwani Pemba.
Aliwapongeza wanachama wajumbe wote
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kumuamini kasha kupendekeza ateuliwe
kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM Tanzania, na akaahidi kuwa atatumia nafasi
yake kuleta mageuzi makubwa ya kimaendeleo ndani nan je ya CCM.
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla (Mabodi), alisema kazi kubwa ya Chama cha
mapinduzi kwa zama za sasa ni kutekeleza kwa vitendo dhana ya CCM mpya na
Tanzania mpya kwa maendeleo ya jamii.
Alisema miradi mbali mbali ya
maendeleo iliyotekelezwa kwa ufanisi kisiwani Pemba ikiwemo mfuko wa maendeleo
wa TASAF na kuongeza bei ya zao la karafuu ni kutokana na utekelezaji mzuri wa
sera za CCM.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Kusini Pemba Ndugu Yussuf Ali Juma alisema ndani ya Mkoa huo wanaendelea na
mikakati ya kuhakikisha CCM inashinda kwa ngazi zote katika uchaguzi Mkuu ujao.
Katika ziara hiyo Dk. Bashiru
alifuatana na viongozi mbali wa Chama na Jumuiya wakiwemo wajumbe wa Kamati Kuu
ya CCM Taifa, wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Makamu Wenyeviti wa
Jumuiya pamoja na viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali Zanzibar.
Dr Bashiru: hakuna Chama chochote cha kisiasa nchini kinachoweza kushindana CCM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 20, 2018
Rating:
![Dr Bashiru: hakuna Chama chochote cha kisiasa nchini kinachoweza kushindana CCM](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9Ek71erOY50JKpiS_hXvKfrCB6xyIAkD6qCEmSt_eFKb6_Tnh_JNdEB56O9Su_pJ5AWZyGUslHviw0QoQdZAsR4wtVQmJBhF_EQsfAu2dC9xuACIh6zLeXXF-MFE-Nv5diEt4BCvQfQE/s72-c/1F.jpg)
No comments:
Post a Comment