Anaswa na Gramu 300 za dawa za Kulevya


Dar es Salaam. Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) inamshikilia mkazi wa Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam, Mohamed Hussein Gulam (48) kwa tuhuma za kukutwa na gramu 300 za dawa za kulevya zinazodhaniwa kuwa ni heroin

Kamishna wa Intelijensia wa mamlaka hiyo, Fredick Kibuta amezungumza akisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Agosti 16, 2018 saa 9 usiku nyumbani kwake akiwa na dawa hizo alizokuwa akiziandaa kwa ajili ya kuziuza

Amesema baada ya kuzikamata walifanya vipimo vya awali na kuonyesha unga huo ni dawa za kulevya aina ya heroin hivyo wameupeleka kwa mkemia mkuu wa serikali ili kubaini aina gani ya dawa za kulevya iliyokamatwa

"Mtuhumiwa bado tunamshikilia tunasubiri majibu kutoka kwa mkemia mkuu wa Serikali yakikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufikishwa mahakamani," amesema Kibuta

Amesema Gulam alianza biashara ya kuuza dawa za kulevya aina ya heroin mwaka 1995 akiwa anaishi nchini Italia ambapo alikuwa akiagiza dawa hizo nchini Pakistani na kuzisambaza nchi mbalimbali

Mwaka 1999 alirudi nchini huku akiendelea na biashara hiyo na alikuwa akishirikiana na washirika wake kutoka Nigeria alikokuwa anauza kwa rejareja na jumla

 Amezitaja baadhi ya nchi alikokuwa anaziuza dawa hizo kuwa ni Uturuki, Italia, Afrika Kusini, India na Kenya huku akiwatumia watu wake ambao walikuwa wanasambaza
Kibuta amesema Julai 18, 2018, mamlaka hiyo ilimkamata mkazi wa Kagera jijini Dar es Salaam, Islem Shebe Islam akiwa na gramu 306 za heroin, Julai 20, 2018 alikamatwa mkazi wa Ununio jijini humo, Mfungeni Azizi Mohamed akiwa na gramu 215 aina ya heroine na gramu 3.15 aina ya cocaine na Agosti 14, 2018 alikamatwa Ally Yusuph maarufu Porojo akiwa na gramu 300 za dawa aina ya heroin

Anaswa na Gramu 300 za dawa za Kulevya Anaswa na Gramu 300 za dawa za Kulevya Reviewed by KUSAGANEWS on August 20, 2018 Rating: 5

No comments: