Askari wanne wa Pori la Akiba
la Mkungunero, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kiteto
kwa tuhuma ya kushawishi na kuomba rushwa ya Sh milioni tano kutoka kwa
wafugaji ambao mifugo yao ilikamatwa ndani ya pori hilo.
Akisoma hati ya mashtaka ya
watuhumiwa hao, Mwendesha mashataka wa Takukuru Mkoa wa Manyara, Isdory Kyando
mbele ya Hakimu Mkazi, Hudi Majid, alidai tukio hilo lilitokea Mei
12 mwaka huu katika Kijiji cha Ilkiushbouir wilayani Kiteto.
Kyando aliwataja watuhumiwa hao kuwa
ni Martenus Mahoka, Augustino Sadick, Ephrahim Polepole na Godfrey Matheas wote
askari wa Pori la Akiba la Mkungunero.
Alidai fedha hizo waliziomba kutoka
kwa wenye mifugo waliokuwa wamekamatwa ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero
waweze kuiachia mifugo199 wakiwamo ng’ombe, mbuzi, kondoo na punda.
Kyando alidai washtakiwa hao kwa
pamoja wanatuhumiwa kutenda kosa kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa namba 11/2007 kifungu cha 15 (1),
Washtakiwa hao kwa
pamoja walikana mashitaka na walipata dhamana hadi Septemba
17 mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena
Askari Wanne Kortini Kwa Kuomba Rushwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 20, 2018
Rating:
![Askari Wanne Kortini Kwa Kuomba Rushwa](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhTmt0-uLUk1g_g6s25Viou2e3Prl74QiIWDWQA4wkwMAowmmYaoPcvKQVBSUA2wcxCpwlBRjfmlHZL9e5AuQrFfx7kTo5fDnm04qfNMaAc1_1ZELg4k6mBXFL85PMYUSt7a-gZmMTaOug/s72-c/%255BUNSET%255D.png)
No comments:
Post a Comment