MAHAKAMA ya Wilaya ya Lindi imemuhukumu Mussa Milanzi (29),
kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kiume
mwenye umri wa miaka mitano
Hakimu wa mahakama hiyo Erasto Phili, alitoa hukumu hiyo
baada ya kuridhika na ushahidi wa kitaalamu wa idara ya afya na upande wa
mashtaka
Kabla ya hukumu hiyo mshtakiwa huyo alitoroka baada ya
kupewa dhamana na kwenda kujificha Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara, ambako
alikamatwa na kurejeshwa mkoani Lindi
Awali Mwanasheria wa Serikali, Yahaya Gumbo aliiambia
mahakama hiyo kwamba Oktoba 11, mwaka jana mchana, mshtakiwa akiwa kwenye kazi
yake ya kuchunga ng'ombe eneo la pori la Angaza, Manispaa ya Lindi, watoto
walikuwa wakimfuata nyuma na mifugo yake ndipo alipomkamata mmoja wao na
kumlawiti
Mshtakiwa huyo alipotakiwa kujitetea, aliiomba mahakama
imuonee huruma kwa kuwa ana mke na mtoto mchanga na kwamba akipewa adhabu hiyo
watakosa huduma yake
Alidai kuwa alifanya kitendo hicho kutokana na kupitiwa na
upepo mbaya
Baada ya utetezi huo, Mwanasheria wa Serikali Yahaya Gumbo,
aliiomba mahakama kumpa mshtakiwa huyo adhabu kali ili iwe fundisho kwake na
wengine wenye tabia kama hiyo, ikizingatiwa amefanya unyama huo kwa mtoto asiye
elewa kitu chochote
Hakimu Phili akitoa hukumu hiyo alisema licha ya utetezi
huo, kitendo cha kinyama alichomfanyia mtoto huyo asiye na hatia hakiwezi
kuachiwa kiendelee
Afungwa Jela Milele kwa Kulawiti Mtoto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 20, 2018
Rating:
![Afungwa Jela Milele kwa Kulawiti Mtoto](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgnBveMs0kzjrXQgrZQUaCsmmdJoz-ICTaMTH1v7-okasjcEj0lRPz4Lay5N1owtINSH-ZUmyCreGUPsx7rGDttcgiD-i2bgsuEHKvJuSSL3zd1hSdC5kB7VIukIqhbzRccybTGbcanPes/s72-c/_102724617_f3a6e0af-b193-49f8-8120-a541cbec159a.jpg)
No comments:
Post a Comment