Serikali imewataka Wananchi wa Wilaya ya Longido Mkoani
Arusha kuchukua Tahadhari mapema kwa kuwa na tabia ya Kuhifadhi chakula ili
kipindi cha Ukame wasilie njaa kwa kuwa Wilaya hiyo imebarikiwa kuwa na maeneo
ambayo ni mazuri kwa kilimo na ufugaji.
Hayo yamesema na mkuu wa wilaya ya Lingido Mh Frank
Mwaisumbe wakati alipotembelea na kukagua Ghala la Kuhifadhia nafaka katika
tarafa ya Engarenaibo mradi ambao umegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 100
mpaka ulipokamilika ambapo unasubiria Mwenge kwa ajili ya kuzinduliwa.
.
Mwaisumbe amesema kuwa serikali inahakikisha inajali
wananchi wake ndiyo mana ikatoa Fedha hizo ili kuleta mradi huo ambapo amewaomba
wananchi kutumia Fursa Hiyo ambayo inaletwa na Serikali ya awamu ya Tano Chini
ya Raisi Dkt John Pombe Magufuli.
Amesema kuwa mradi huo utawasaidia
wananchi kioindi cha ukame pamoja na kupunguza gharama kubwa ya kununua Chakula
.
Ameongea kuwa licha ya kuwa jamii inayoishi wilayani
Longido Wengi ni Wafugaji ni vema wakatumia Fursa ya Kununua Chakula na
Kuhifadhi kwa kuuza baadhi ya Mifugo ambayo italeta faida kwa kuwa na chakula
kuliko kusubiri kipindi cha Ukame ambacho Mifugo ufariki kwa Kukosa Malisho.
Dc Longido "Wananchi wa Longido Chukueni Tahadhari Kuhifadhi Chakula"
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment