DC Mpya Longido awaweka kati wawekezaji wa Madini waliokuwa na Mgogoro wa Muda mrefu


Mkuu wa Wilaya ya Longido ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Frank Mwaisumbe amemaliza mgogoro uliyokuwepo kati ya Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Sendeu Inverstment LTD na Mundarara Group Mining iliyopo eneo la Mundarara eneo ambalo ni maarufu kwa auchimbaji wa madini ya Ruby ambao umedumu kwa muda mrefu bila Maelewano.

Akizungumza na Kusaga News Ofisini Kwake Mkuu Huyo Bwana Mwaisumbe amesema kuwa baada ya agizo la waziri wa madini Mh Angela Kairuki aliagiza mgogoro huo ufanyiwe kazi na Ashughulikiwe mara moja ili shughuli za uchimbaji ziendelee
 
Mwaisumbe Amesema kuwa baada ya agizo hilo aliunda kamati ya Uchunguzi kwa ajili ya kushughulikia mgogoro wa kampuni hizo mbili za uchimbaji wa madini na hatimaye leo Agost 17 ,2018 amekutana na pande zote mbili na kutoa maagizo ambayo watayatekeleza ili kumaliza Mgogoro huo wa wachimbaji wa migodi hiyo.

Ameongeza kuwa katika kikao hicho cha usuluhishi wa pande mbili kama serikali wametoa maagizo kumi ambayo yote yamekubaliwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi na kuahidi ushirikiano baina yao kama wawezekazaji kwasababu serikali bado inahitaji wawekezaji ili kupata maendeleo zaidi.

Hata hivyo ametoa wito kwa wamiliki wa madini kutumia nga\zi hudika katika kutatua migogoro kwakua hapo awali walikuwa wanawatumia watu ambao hawahusiki kama wanasiasa wasaatu ambao hawawezi kuwasaidia huku akiwataka wawezaji kujitokeza kushirikiana na serikali kwasababu maeneo ya uwekezaji bado yapo na vibali vinapatikana.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa kampuni ya Sendeu Inverstment Ltd Gabriel Sendeu Laizer ambaye walikuwa na Mgogoro na Kampuni ya Sendeu Mining amemshukuru Mkuu wa Wilaya Mh Mwaisumbe kwa kumaliza mvutano uliyokuwepo kwasababu ulikuwa unaikosesha pia serikali mapato stahiki na kuahidi kushughulikia yote walioagizwa kuyafanya.

Sendeu amesema kuwa kinachofanyika kwasasa ni kufanya vipimo ambavyo vitasaidia wao kutoingiliana katika mipaka ambayo inatenganisha Maeneo ya wawekezaji hao wawili ambapo wao walitoboa upande wa kampuni ya Sendeu mining.

Naye Muwekezaji wa kampuni ya Mundarara Miningi amesema kuwa mgogoro huo umemalizika kwa amani na wataendelea kushirikiana kwa pamoja kwasababu mgogoro huo ulisababisha kupunguza mapato ya kijiji kwa zaidi ya asilimia 90.



DC Mpya Longido awaweka kati wawekezaji wa Madini waliokuwa na Mgogoro wa Muda mrefu DC Mpya Longido awaweka kati wawekezaji wa Madini waliokuwa na Mgogoro wa Muda mrefu Reviewed by KUSAGANEWS on August 17, 2018 Rating: 5

No comments: