Mambo yamekuwa mambo mitandaoni. Ndivyo unavyoweza kusema
kutokana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Kiongozi
wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kuvutana katika mtandao wa kijamii wa Twitter
kuhusu mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri
Katika mabadiliko hayo yaliyofanywa na Rais John Magufuli,
Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ameachwa
Zitto aliandika katika ukurasa wake, “ndugu yangu Mwigulu
Nchemba karibu back bencha ufanye kazi ya wananchi. Tunajua msimamo wako kuhusu
barua ya KKKT (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania) umekuponza, ulikuwa na
msimamo madhubuti na ulisimamia haki.”
Baada ya Zitto kuandika hayo, Polepole aliibuka na kumjibu,
“mzee wa kurukia treni kwa mbele ushaanza, mbona unapenda ubashiri na vitendo
vya kilozi. Rais hutenda impendezavyo kwa dhamana aliyopewa na Katiba.”
“Sisi tuliohudumu kwenye serikali na chama tunajua na
kuheshimu, usijitatafutie huruma kwa mtu acha kupotosha hiyo si siasa safi.”
Katika mabadiliko hayo, nafasi ya Mwigulu imechukuliwa na
Kangi Lugola ambaye awali alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira).
Zitto, Polepole wavutana mtandaoni kisa Mwigulu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment