Watu
11 wa familia moja wamepatikana wakiwa wamekufa kwenye nyumba iliyo katika mji
mkuu wa India Delhi, huku 10 kati yao wakiwa wananing'inia katika dari la
nyumba hiyo, kwa mujibu wa polisi.
Mwanamke mmoja aliye na takribani
miaka 70 alipatikana kwenye sakafu ya nyumba. Wengi wa wale waliokuwa wamekufa
walikuwa wamefungwa macho na mikono nayo ilikuwa imefungwa kwa kamba mgongoni.
Familia hiyo imeishi wilaya ya
Burari mjini Delhi kwa zaidi ya miaka 20 licha ya kwamba wametokea katika
maeneo ya Rajathan uku familia hiyo ikiwa inamiliki maduka mawili katika
ghorofa ya chini kwenye jengo la ghorofa tatu.
“Nilipokuwa naenda dukani niliona
mlango ukiwa umefunguliwa na nilipoingia ndani niliona miili ya watu hao ikiwa
imening’inia katika dari uku imefungwa mikono kwa nyuma” amesema Gurchan Sigh alipokuwa akiojiwa na moja ya chombo
cha habari mjini Delhi.
Uku taarifa ya awali kutoka polisi
inazungumzia karatasi zenye maandishi walizozipata kwenye nyumba hiyo ambazo
zinaashiria kufanyika kwa matambiko yanayoonekana kuwa na uhusiano na vifo
hivyo.
“bado tunasubiri matokeo ya
upasuaji, na kuwahoji majirani na kuchunguza video za CCTV eneo hilo” amesema afisa mmoja wa polisi alipokuwa akizungumza na chombo
cha habari uko mjini Dehli..
Sababu za mauaji hayo pamoja na
wahusika bado hazijawekwa wazi na polisi mjini Delhi imesema kutoa taarifa
baada ya uchunguzi kufanyika.
Watu 11 wa familia moja wanyongwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment