Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amefanikiwa kutaifisha vifaa vilivyokuwa
vikitumiwa na wahalifu katika pori la msitu wa Patamela baada ya kuhofia
kukamatwa.
Hayo
yamebainishwa na Waziri Kigwangalla ambaye yupo katika ziara ya pori kwa pori
mkoani Songwe ambapo amebainisha kuwa baada ya wahalifu hao ambao walikuwa
wakifanya ujangili katika machimbo ya madini walichoma moto na kutelekeza vifaa
vyao kisha kutoroka.
Akisimulia
tukio Waziri amesema " Kwenye ziara yetu wilayani Songwe, Mkoa
wa Songwe, kwenye msitu wa Patamela, ambao ni msitu wa asili wa hifadhi wa
kitaifa unaochukua sehemu kubwa ya wilaya za Songwe na Chunya, tulikuta kuna
ujangili wa uchimbaji madini ulioshamiri, wahalifu walichoma moto ili
kutuchelewesha tusifike eneo la tukio waweze kuondoka".
Ameongeza,
"Bahati nzuri, tulipambana kwa ushirikiano wetu wote tuliokuwepo na
tulifanikiwa kuudhibiti moto na kuendelea na safari mpaka eneo lililovamiwa na
wachimbaji haramu wa madini. Tuliwawahi wakakimbia wakatelekeza vifaa na
mashine (wheel loader) ambayo tumeitaifisha, sambamba na makinikia yote".
Hata hivyo
Kigwangalla amesema kazi bado inaendelea na ziara ya pori kwa pori
inaendelea ambapo leo atakuwa Chunya mkoani Mbeya.
Kigwangalla awashiwa moto na wahalifu msituni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment