Mwenyekiti wa Umoja wa
Vijana CCM (UVCCM) Wilaya ya Tarime, Godfrey Francis leo Jumatatu Julai 2, 2018
amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Tarime,
kushtakiwa kwa kosa la kusambaza taarifa za uwongo kwa njia ya mtandao wa
kijamii.
Taarifa hizo ni kuhusu
kukamatwa kwa mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Zakaria, Peter Zakaria.
Kiongozi huyo ambaye
jana alihojiwa na polisi kwa saa kadhaa amesomewa mashtaka na mwendesha
mashtaka wa polisi, Kazeni Mrita.
Mbele ya hakimu mkazi
Veronica Mugendi, Mrita amedai mshtakiwa amesambaza taarifa hizo mchana wa
Julai Mosi, 2018 kwa kuandika kuwa Zakaria alitaka kutekwa na watu
wasiojulikana ambao hata hivyo aliwazidi nguvu kwa kuwajeruhi wawili kati yao.
Francis anayetetewa na
wakili Onyango Otieno ameachiwa kwa dhamana hadi Julai 30, 2018 shauri hilo
litakapotajwa.
Ametimiza masharti ya
kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja amesaini hati ya dhamana ya Sh2
milioni.
Mwenyekiti UVCCM apandishwa kizimbani, aachiwa kwa dhamana
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment