Aliyekuwa Mbunge wa
Korogwe Vijijini (CCM), Steven Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu,
ataagwa kesho na baadaye mwili kusafirishwa kuelekea jimboni kwake Korogwe
kwaajili ya maziko.
Akizungumza Kaka wa marehemu, Hilary
Ngonyani amesema kuwa taratibu za kuaga mwili wa marehemu zitatangazwa baadae,
ikiwemo mahali itapaofanyika ibaada ya kuaga mwili wa marehemu Maji Marefu,
pindi watakapokamilisha mawasiliano na ofisi ya Bunge.
“Mwili utabaki Muhimbili leo, hadi
hapo kesho tutakapoaga katika viwanja ambavyo taarifa itatolewa badae baadaya
ya kukamilisha mawasiliano na Ofisi ya Bunge, ambapo ataagwa na wakazi wa
Jijini Dar es salaam pamoja na wabunge wenzake na baadaye tutaanza safari ya
kuelekea Korogwe kwaajili ya shughuli ya Mazishi”, amesema Hilary Ngonyani.
Taarifa za kifo cha mbunge huyo
ziliripotiwa usiku wa Julai 2, majira ya saa 3:20 na Ofisa Uhusiano wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha.
June 6, 2018 mbunge huyo alifiwa na
mkewe, Mariam aliyekuwa akipatiwa matibabu hospitali ya taifa pia.
Taratibu za kuagwa na mazishi ya Prof. Maji Marefu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment