Jumla ya watoto 12
pamoja na kocha wao wa Mpira wa Miguu ambao walipotelea pangoni tangu Juni 23
wameonekana wakiwa hai katika moja ya pango lililojaa maji Jimbo la Chiang Rai
nchini Thailand.
Vijana hao wenye umri wa kati ya
miaka 11 hadi 16 pamoja na kocha wao mwenye umri wa miaka 25 wameonekana
mita 400 kutoka eneo ambalo walikuwa wakicheza baada ya kuingia katika pango
moja wakati likiwa kavu na ghafla baada ya muda mvua kubwa ikanyesha na kuwazuia
kutoka katika pango hilo.
Kikosi cha waokoaji wa vijana hao
kimeeleza kuwa kiwango cha maji katika pango hilo ni kikubwa kiasi cha kuleta
ugumu wa kuwatoa vijana hao kwa haraka zaidi lakini juhudi kubwa zinafanyika
kuweza kufanikisha uokoaji kwa haraka iwezekanavyo .
Vijana hao waligunduliwa na kikosi
cha uokoaji cha Uingereza usiku wa Jumatatu baada ya kuombwa kwenda kusaidia
harakati hizo japo juhudi za kuwaokoa kwa haraka zimeshindikana baada ya njia
ya kuyanyonya maji katika pango hilo kushindikana na endapo waokoaji wataamua
kusubiri maji yakauke basi vijana hao watakaa kwa muda wa mwezi mmoja katika
pango hilo.
Kwa mujibu wa jeshi la nchi hiyo,
njia pekee inayoweza kuwanusuru vijana hao kwa haraka zaidi ni kujifunza namna
ya kuogelea ili waweze kutoka au wasubirie mwezi mmoja upite ili maji yapungue
katika pango hilo.
Bonde hilo la Tham Luang limekuwa na
historia ya kujaa maji kipindi cha mvua ambapo mvua hizo huwa zinanyesha hadi
miezi ya Septemba na Oktoba.
Watoto waliopotelea Pangoni wapatikana
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment