Kufuatia kifo cha Mbunge
wa Korogwe vijijini (CCM), Stephen Ngonyani maarufu kama Prof. Maji Marefu
kilichotokea usiku wa kuamkia leo kimeweza kumuibua aliyekuwa Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba na kuunga na viongozi wengine wa CCM katika
kutoa salamu za pole.
Dkt. Mwigulu ambaye amevuliwa nyadhfa
zake na Rais Magufuli mwishoni mwa wiki iliyoisha kupitia mtandao wake wa
kijamii amesema kwamba CCM imepata pigo kubwa kwa kumpoteza kada na kiongozi wa
kweli.
"Maandiko matakatifu yanasema,
mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi. Tumempoteza
kaka, ndugu na rafiki comrade Stephen Hilary Ngonyani(Prof. Maji Marefu),
tumempoteza kiongozi na kada kweli kweli wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM)", ameandika
Mwigulu.
Mbali na Mwigulu, Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa pole zake kwa
familia huku akiwataka wawe na ustamilivu katika kipindi hiki kigumu
walichokuwa nacho.
"Mbele yako, nyuma yetu.
Pumzika kwa amani kaka yetu Stephen Ngonyani (Prof. Maji Marefu). Natoa pole
nyingi kwa familia, ndugu, jamaa na wananchi wa Korogwe Vijijiji. Mwenyezi
Mungu awape ustamilivu katika kipindi hiki kigumu", ameandika Ummy.
Pamoja na hao pia Mbunge wa Jimbo la
Mtama, Nape Nnauye ameguswa na kifo hicho cha kada mwenzao wa CCM na kumuombe
dua marehemu huko aendapo.
"Kaka na rafiki wa kweli,
pumzika kaka", ameandika
Nape.
Mbunge huyo wa Korogwe vijijini,
Steven Ngonyani amefariki akiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini
Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ambayo yaliyokuwa
yanamsibu na kufanya idadi ya Wabunge waliofariki kufikia watano hadi hivi sasa
wakiwemo wanne wa majimbo na mmoja wa viti maalumu.
Mwigulu, Nape na Ummy Mwalimu waungana kwa hili
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment