Kaka wa Mbunge wa
Singida Mashariki, Alute Mughwai amesema wanatarajia kwenda
mahakamani kudai haki ya kisheria ya matibabu ya ndugu yao Tundu Lissu
aliyeshambuliwa na risasi Septemba 07, 2017.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari, Mughwai amesema wanachukua hatua hiyo baada ya
Bunge kuiandikia barua familia hiyo, ikieeleza kuwa kuanzia sasa
haitajishughulisha na matibabu ya mbunge huyo.
Mughwai
amesema Juni 18, 2018 walipokea barua kutoka uongozi wa Bunge kuwa
haitajishughulisha na matibabu ya mbunge huyo kwa kuwa yuko nje ya nchi kwa
utaratibu binafsi na hakufuata utaratibu wa matibabu.
Mughwai
amesema kutokana na hali hiyo wanaangalia utaratibu wa kwenda mahakamani
kuangalia kama mwakilishi huyo anahaki kisheria ya kupatiwa matibabu ama la.
Kwa sasa Tundu
Lissu yupo nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu amabyo kwa mujibu wake na
familia pamoja na chama chake matibabu hayo yanalipiwa na wasamaria wema.
Familia ya Lissu kutinga mahakamani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment