Rais John Pombe Magufuli
amesema alikuwa akisubiri wakulima wa mikoa ya Lindi na Mtwara wafanye fujo
kama jinsi ambavyo Wabunge wa mikoa hiyo walivyokuwa wakidai na kueleza kwamba
angewashughulikia kwa kipigo na angeanza na jimbo linaloongozwa na Waziri Mkuu.
Rais Magufuli
ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa hotuba yake baada ya kuwaapisha Mawaziri
na viongozi wengine ambao aliwateua siku ya jana alipofanya mabadiliko madogo
katika wizara yake.
"Watu
wanataka popularity, wengine nilisikia wanasema watachomewa nyumba, nilimwambia
Waziri Mkuu nataka nione wakifanya fujo. Ningewapa kipigo. Tena ningeanza
kwenye jimbo lake kama kuna shangazi zake ningeanza kupiga hao. Nasema ukweli
wala sifichi"
Rais ameongeza
"Lazima tufike mahali tuambizane ukweli, ndiyo maana nilimwambia
Katibu Mkuu CCM, aende Dodoma siku ya kupiga kura. Wabunge wa CCM ambao
hawakuwepo wachukuliwe hatua".
Katika
kuonyesha kukasirishwa na kitendo ambacho kilifanya na Wabunge wa Mikoa hiyo
ambo pia ni wa CCM, Rais Magufuli amesema anashangaa wanafanya nini mpaka saizi
kwenye Chama Cha Mapinduzi badala ya kuondoka.
"Watu
wanashangilia uongo, tumechoka, nilimuuliza Waziri Mkuu kuna wabunge wangapi wa
CCM, Mtwara na Lindi akasema wapo 17, nikasema bora waondoke wote, hata Waziri
Mkuu ni wa huko naye angeondoka, bado tungeweza kuongoza nchi. Nilimpigia simu
Katibu wa CCM tukae kwenye mpango huo. Wangeondoka,
"
Pamoja na
hayo, Rais Magufuli amesema "Siku ya kupitisha bajeti nikamwambia
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru nenda Bungeni ukaangalie wabunge wangapi wa
CCM hawapo bungeni uwalime barua, na kweli amewaandikia barua wote. Japo wapo
Wabunge waliokuwa na sababu za Msingi lakini kuna wale ambao wamelimwa barua.
Prof. Kabudi alikuwa amelazwa lakini kapokea barua yake na ataambatanisha na
vyeti vya hospitali"
Mbali na hayo
Rais amempongeza Naibu Waziri Mpya wa Kilimo na Umwagiliaji kwa kuweza
kupambana kuitetea serikali wakati wa hoja ya Korosho ilipokuwa imepamba moto.
"Naibu
Waziri wa Kilimo nakupongeza kwa kazi uliofanya Bungeni, huwa nafuatilia
michango ya CCM, mwingine anasema tukienda hivi tutashindwa, kwa nini bado uko
CCM, si utoke huko? Nakuomba ukashirikiane na wenzako Wizara ya Kilimo"
amesema.
"Ningeanza kipigo na Shangazi wa Waziri Mkuu"- JPM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment