Katibu wa Itikadi,
Mawasiliano na Uenezi ACT Wazalendo, Ado Shaibu amefunguka kuwa hakuna
mwanaharakati anayeweza kulitetea Taifa akiwa chini ya Chama tawala.
Shaibu amefunguka hayo katika
mkutano wa wake na wanahabari leo, katika ofisi za Chama hicho ambapo amesema
kuwa endapo wabunge, Nape, Bashe na Hawa Ghasia wana nia ya dhati ya kuwatetea
wanyonge wahamie ACT-Wazalendo.
“Wabunge wanaotetea haki za
wanyonge, wakina Nape, Bashe na Hawa Ghasia haiwezekani kufanya harakati za
kuwatetea wanyonge huku mkiwa CCM, sana sana mtaonekana waasi katika chama
chenu njooni kwetu”, amesema
Shaibu.
Hayo yamejiri ikiwa ni siku chache
kabla ya kuahirishwa kwa vikao vya Bunge, liliibuka sakata la korosho
lililokuwa likiendelea katika vikao vya Bunge, ambapo Wabunge wa CCM ambao
waliokuwa wakilipigia kelele suala hilo ni Hussein Bashe, Nape Nnauye pamoja na
Hawa Ghasia.
Nape, Bashe na Hawa Ghasia wapewa nafasi ACT
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment