Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ngenya Athuman Yusuf kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Ngenya Athuman Yusuf umeanza tarehe 30 Juni, 2018.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Ngenya Athuman Yusuf alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).

Dkt. Ngenya Athuman Yusuf amechukua nafasi ya Prof. Egid Beatus Mubofu ambaye ameteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine   Reviewed by KUSAGANEWS on July 03, 2018 Rating: 5

No comments: