Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko ya makamanda wa polisi
kwa baadhi ya mikoa
Taarifa kwa
vyombo vya habari iliyotolewa leo Julai 3, 2018 iliyosainiwa na Msemaji
wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa, inasema mabadiliko hayo yanalenga
kuongeza juhudi za kuzuia ajali zilizotokea mara kwa mara katika baadhi ya
mikoa.
Katika
mabadiliko hayo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Deusdedit Nsimeki
aliyekuwa makao makuu ya upelelezi Dar es Salaam anakwenda kuwa Kamanda wa
Polisi (RPC) Mkoa wa Simiyu
Aliyekuwa RPC
Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei
anakwenda kuwa RPC Mkoa wa Mbeya
Katika
mabadiliko hayo, aliyekuwa Kaimu RPC Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi,
Mussa Taibu amehamishiwa makao makuu ya polisi Dar es Salaam
Aliyekuwa RPC
Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa
anakwenda kuwa RPC Mkoa wa Morogoro, nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna
Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Nley kutoka makao makuu ya polisi Dar es Salaam
Wengine
waliohusika na mabadiliko hayo ni aliyekuwa Ofisa Mnadhimu Mkoa wa Geita
Kamishna Msaidizi wa Polisi, Stanley Kulyamo anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi
Kikosi cha Tazara
IGP Sirro
amewataka makamanda wa polisi wa mikoa nchini, kuendelea kuwajibika ipasavyo
katika kuhakikisha ajali hazitokei katika maeneo yao na kuwachukulia hatua kali
madereva watakaosababisha ajali kwa uzembe.
IGP Sirro apangua makamanda polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment