Abiria 120 walala kituo cha polisi


Abiria zaidi ya 120 waliokuwa wakisafiri na magari mawili ya kampuni ya King Msukuma walilazimika kulala kituo cha Polisi jana Julai 2 baada ya kukamatwa na Polisi wa usalama barabarani kutokana na ubovu

Magari hayo yalikamatwa jana saa 11 jioni yakiwa safarini kutoka Mwanza kwenda Kagera na jingine kutoka Kagera kwenda Mwanza
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 3, kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema magari hayo 

yamekamatwa katika operesheni inayoendelea ya ukaguzi wa magari yanayoingia na kutoka katika kituo kikuu cha magari mjini Geita
Kamanda Mwabulambo amesema katika operesheni waliyofanya jana magari 59 yalikaguliwa na 47 yalikutwa na makosa madogo na kutozwa faini

Amesema magari mawili ndiyo yaliyokamatwa na kuzuiwa lakini leo asubuhi walipakiwa kwenye magari mengine na kuendelea na safari zao.
Abiria 120 walala kituo cha polisi Abiria 120 walala kituo cha polisi Reviewed by KUSAGANEWS on July 03, 2018 Rating: 5

No comments: