Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi) imewataka wataalam wa afya 6,180 walioajiriwa kuripoti katika vituo
vyao ya kazi ndani ya siku 14
Wataalam hao wa afya watasambazwa katika vituo vya
afya, hospitali za Wilaya na zahanati nchini.
Akizungumza leo Juni 9, 2019 na Waziri wa Tamisemi, Selemani
Jafo amesema atakayeshindwa kuripoti ndani ya muda huo, ajira yake atapewa
mwingine
Mei 10, 2018 Jafo alitangaza nafasi za ajira hizo na
kubainisha kuwa watumishi watakaoajiriwa watapangiwa kwa kuzingatia mahitaji,
kuwataka wenye sifa za taaluma katika kada ya afya wajitokeze kuomba nafasi kwa
lengo la kutoa huduma kwa wananchi
“Wasijikusanye katika ofisi za mjini kwasababu
hatutabadilishia vituo kwa kuwa walipoomba ajira walisema wapo tayari kufanya
mahali popote ndani ya Tanzania," amesema Jafo leo
Jafo amesema upangaji wa watumishi hao umezingatia
halmashauri ambazo zina zahanati na vituo vya afya lakini hazina watumishi,
vituo vya afya 210 ambavyo vilikarabatiwa na zahanati ambazo zilikuwa
zinaongozwa na wahudumu wa afya
Ametaka wananchi kuwapokea wahudumu wa afya ili wawatumikie
na waache kuwafanyia mambo mabaya kama katika baadhi ya maeneo ilivyokuwa
ikifanyika
Amesema majina ya walioajiriwa yanapatikana katika tovuti ya
Tamisemi
Wataalam wa afya 6,180 wapangiwa vituo vya kazi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment