|
Mbunge wa jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni naibu waziri
wa elimu sayansi na teknolojia William Olenasha akiwa na wananchi wake wa
kijiji cha Orkuyene wakati wa alipofanya ziara katika eneo hilo
|
|
Wanawake wajasiriamali kijiji cha Erkuyene wakifurahia
baada ya kutembelewa na mbunge wa Jimbo la Ngorongoro William Olenasha
|
|
Msafara wa wananchi wa kijiji cha Erkuyene tarafa ya
Longido wakiwa wanampokea Mbunge wao alipowatembelea
ikiwa ni muendelezo wa ziara yake
|
|
Wanafunzi na wananchi waliofika kumsikiliza Mbunge wao
aliyefika kijiji cha Erkuyene tarafa ya Longido kwa ajili ya kuwasikiliza
wananchi wake
|
Wameyasema hayo wakati wakizungumza kwenye mkutano wa
harambee ya kuchangia vikundi vya wanawake wajasiriamali wadogo wadogo zaidi ya
100 ambapo zilipatikana zaidi ya shilingi Milioni 22 katika kijiji cha Orkuyene
tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro.
Katika harambee hiyo ambayo iliendeshwa kwa masaa manne na
Mbunge Olenasha ambaye ametoa shilingi Milioni 4 kwa ajili ya akina mama hao zilipatikana
zaidi ya shilingi Milioni ishiriki mbili ambazo zitawasaidia wajasiriamali
ambao wameamua kujiajiri ili kujipatia kipato.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mmoja wa akina mama
mjasiriamali Kijoa Lepuluka amesema kuwa wamempata mbunge ambaye kama
angekuwepo kwa tangu mwanzo wangekuwa na maendeleo zaidi ya walionayo sasa
hivi.
“Kweli tunamshukuru sana Mbunge wetu mana ametuletea
mabarabara ,Umeme na amejitolea kutusaidia sisi wamama kwakweli tungekuwepo
naye tangu nyuma tungekuwa mbali na huyu atakuwa mbunge wetu mpaka atakapoacha
mwenyewe” amesema Kijoa Lepuluka
Naye Meseyi Mejoli amesema kuwa Mbunge wao amekuwa
akiwapa ushirikano hata anapopigiwa simu anapokea kwa wakati na kama kuna
tatizo linapata ufumbuzi kwa wakati.
Kwa upande wa Mejool Maisii amesema kuwa kwa kipindi
kirefu wamekosa maendeleo kwasababu viongozi waliopita walikuwa hawajali
maslahi ya wananchi wao waliowachagua lakini Mbunge wao wasasa msaada mkubwa.
Amesema kwasasa hawataki siasa chafu ambazo zinaweza
kuwarudisha nyuma kimaendeleo na kwamba hawana shida na mbunge mwingine tofauti
na olenasha ambaye amewaletea barabara ya Lami,Maji,Umeme na madarasa.
Mbunge Olenasha bado anaendelea na ziara yake ya
kutembelea wananchi wa jimbo lake ili kuwaeleza mafanikio aliyoyafanya kama
mmbunge na Serikali ya awamu ya Tano inayosimamiwa na Raisi Magufuli.
Wananchi Ngorongoro wamkubali Olenasha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment