Timu ya wazamiaji leo imefanikiwa kumwokoa mtoto wa tano
kati ya 12 walionaswa kwenye pango nchini Thailand hatua ambayo inazidisha
matumaini ya uwezekano wa kuokolewa watoto wote
Mtoto huyo amesafirishwa kwenda kuungana na wenzake wanne
walioko katika hospitali moja wakichunguzwa afya zao. Kumekuwa na shangwe na
nderemo kutoka kwa wananchi walioshuhudia helikopta ikiruka kutoka eneo la
tukio kuelekea hospitali
Jana, watoto wanne waliokolewa katika operesheni iliyotajwa
ya hatari na changamoto nyingi. Watoto hao na kocha wao wamekuwa katika pango
hilo kwa muda wa wiki mbili sasa
Wazamiaji wamekuwa wakiendelea na kazi hiyo kujaribu
kuwaokoa watoto hao waliosalia huku wazazi wa watoto hao wakiwa katika hali
ngumu kusubiri kama watawapokea wapendwa wao hao
Mamilioni ya lita za maji yamekwisha kutolewa kutoka ndani
ya pango hiloili kurahisisha kazi ya uokoaji. Kazi hiyo inaharakishwa kufuatia
utabiri wa hali ya hewa unaodai kwamba huenda mvua kubwa itanyesha jambo ambalo
litasababisha ugumu wa kazi ya kuwaokoa watoto hao
Kiongozi wa kikosi cha uokoaji ambaye gavana wa jimbo la
Chang Raiu Narongsak Osottanakorn, amesema uokoaji huo wenye mazingira ya
hatari utawachukua muda zaidi
Jinsi mtoto alivyookolewa pangoni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment