Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA),
Godbless Lema amefunguka kuwa sio kila tafiti zinatakiwa kupokelewa kwa furaha
bila kutafakari faida na hasara zake huku akiutilia mashaka utafiti wa Taasisi
isiyo ya kiserikali inayojihusisha na utafiti nchini Tanzania ya TWAWEZA.
Akizungumza Lema
amesema kuwa utafiti wa Twaweza anautilia mashaka kwakuwa umeonekana kutoa
faraja upande mmoja na kuongeza kuwa huenda taasisi hiyo imefanya hivyo kwa
maslahi binafsi.
“Utafiti wa TWAWEZA unapaswa kutiliwa
mashaka hata kama unatoa faraja kwa kiasi fulani dhidi ya washindani wetu
kisiasa,ninafikiri TWAWEZA wanatafuta zaidi uhalali kwa ajili ya siku za usoni
kwa manufaa ya taasisi yao na Serikali”, amesema Lema.
Kulingana na ripoti ya TWAWEZA
inadai kuwa uhuru wa kutoa maoni kwa wananchi umepungua tofauti na miaka mitatu
iliyopita, huku msaada wa demokrasia ya wingi unaendelea kuwa na nguvu ambapo
zaidi ya asilimia 84% wanapendekeza mfumo wa vyama vingi vya siasa.
“Sio kila tafiti ya kupigiwa makofi”-Lema
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment